31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

JENERALI MWAMUNYANGE ATEULIWA KUCHUNGUZA GHASIA ZA UCHAGUZI ZIMBABWE

|Harare, Zimbabwe



Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange, ameteuliwa na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, kwenye tume ya uchunguzi wa vurugu baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Agosti Mosi mwaka huu.

Kutokana na matukio yaliyotokea baada ya uchaguzi wa Agosti ambayo yalisababisha baadhi ya watu kupoteza maisha na uharibifu wa mali, Rais Mnangagwa, amesema katika kutimiza yale anayotakiwa kufanya ili kushughulikia jambo hilo kwa njia ya uwazi na kwa maslahi ya umma ameunda tume ya uchunguzi yenye wajumbe saba kuchunguza unyanyasaji huo uliofanyika wakati wa uchaguzi.

Tume hiyo imeundwa na wajumbe kutoka ndani na nje ya Zimbabwe, kikanda na wa kimataifa waliochaguliwa kwa mujibu wa sharia ya tume ya uchunguzi (sura ya 10:07).

Pamoja na Mwamunyange, wajumbe wengine ni Rais Mstaafu wa afrika Kusini, Kgalema Motlanhte, Rodney Dixon QC (Uingereza), Katibu Mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Madola, Emeka Anyaoku, Wahadhiri wa Chuo Kikuu Zimbabwe, Profesa Charity Manyeruke, na Profesa Lovemore Madhuku na Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Zimbabwe, Vimbai Nyemba.

Aidha Rais Mnangagwa ameainisha majukumu ya tume hiyo ya uchunguzi ikiwamo kuwatambua waasisi na viongozi wa vurugu hizo wakati wa uchaguzi, kuweza kutambua kiwango cha uharibifu na majeruhi na kutoa mapendekezo muhimu juu ya matukio hayo ili yasijirudie katika uchaguzi ujazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles