27.4 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

Jenerali Mwamunyange aagiza Dawasa kumaliza tatizo la maji

Tunu Nassor, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange, ameuagiza uongozi wa mamlaka hiyo kuongeza juhudi katika kujenga vituo vya uchakataji wa maji taka kwa maeneo ya pembezoni ili kutatua changamoto iliyopo.

Akizungumza katika ziara ya Bodi ya Wakurugenzi jana, Jenerali Mwamunyange amesema mamlaka hiyo inafanikiwa kiasi kikubwa katika kupeleka maji kwa wananchi hivyo kinachotakiwa ni kuongeza vituo vya kuchakata majitaka.

Amesema kuzalisha maji mengi kunahitaji pia kuweka miundombinu ya uondoshaji na uchakataji wa maji yanayotumika.

“Moja ya ufumbuzi wa kupunguza tatizo la majitaka ni kujenga vituo vingi vya uchakataji kwa maeneo ya pembezoni ambalo ni jukumu la Dawasa ni kuondoa maji taka baada ya kutumika.

“Hata hivyo, mamlaka ina mipango ya kujenga vituo vingi vya kuchakata majitaka karibu na wananchi jukumu ambalo limekabidhiwa watendaji wa Dawasa,” amesema. 

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema wataanza ujenzi wa vituo vya kuchakata majitaka katika maeneo ya Mashine ya Maji, Kata ya Mtoni na Mikocheni na maeneo mengine.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,672FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles