26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

JENERALI MABEYO AWAPA NENO WAZAZI

NA AMON MTEGA,-SONGEA.

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, amewashauri wazazi kuwaelimisha watoto wao wasijiingize kwenye matendo maovu ambayo yanasababisha Taifa kuingia kwenye  viashiria vya uvunjifu wa amani.

Jenerali Mabeyo, alitoa wito huo jana mjini Songea mkoani Ruvuma, wakati akihitimisha tamasha la siku ya kumbukizi ya mashujaa waliyonyongwa kwenye vita vya Majimaji na Wajerumani  mwaka 1906 -1907, ambapo mashujaa 67 walinyongwa  hadharani wakitetea nchi yao.

Alisema  hivi sasa kumekuwapo baadhi ya vijana wanaojiingiza kwenye vitendo viovu kulingana na utandawazi wa kidunia kinyume na mila na desturi za makabila yao.

Alisema ili kukabiliana na hali hiyo, wazazi wanatakiwa kuendelea kuwaelimisha namna ya umhimu wa kulinda amani kwa kuwa wazalendo kama walivyofanya mashujaa waliopigana vita hiyo.

 

Inaendelea…………… pata nakala yako ya gazeti la #MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles