30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jenas: Solskjaer si sahihi kuifundisha Man United

LONDON, ENGLAND

KIUNGO wa zamani wa timu ya taifa ya England, Hermain Jenas, amesema klabu ya Manchester United ilikosea kumteua Kocha Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Solskjaer, ambaye ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1999, akiwa kama mchezaji wa timu hiyo, alirithi mikoba ya Jose Mourinho Desemba mwaka jana.

Kocha huyo alishinda michezo 10 kati ya 11 ya mwanzo tangu alipokabidhiwa timu hiyo, lakini hadi sasa amepoteza michezo mitano kati ya saba.

Wakati akihojiwa na Shirika la Habari la BBC, Jenas, ambaye pia aliwahi kucheza katika timu ya Tottenham, alisema klabu hiyo ilikurupuka kumpa kibarua cha moja kwa moja kocha huyo.

Solskjaer alikabidhiwa timu hiyo wakati ikiwa nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, wakiwa na tofauti ya pointi 11 dhidi ya timu iliyokuwa nafasi ya nne, lakini timu hiyo bado imebaki nafasi ile ile ikiwa na tofauti ya pointi nne dhidi ya Arsenal, ambayo iko nafasi ya nne.

Kocha huyo alionyesha uwezo mkubwa baada ya kikosi chake kutoka nyuma wakiwa wamefungwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, uliochezwa Uwanja wa Old Trafford dhidi ya PSG na baadaye kushinda mabao 3-1 kwenye uwanja wa ugenini.

Mbio zao katika michuano hiyo ziliishia kwa Barcelona, baada ya kufungwa jumla ya mabao 4-0 na kushindwa kutinga hatua ya nusu fainali.

Kutokana na kushuka kwa kiwango cha timu hiyo, Solskjaer alisema wachezaji wake wanahitaji uangalizi wa kina.

“Hapana, nafikiri walimuajiri kwa hisia kwa maana katika maamuzi ya kibiashara walitakiwa kuangalia mambo mengi ili kumpa mkataba wa moja kwa moja.

“Kitu wanachotakiwa kukiondoa kwa sasa imani yao kwamba timu inacheza katika mtindo wake, jambo ambalo si kweli.

“Kitu alichokifanya Sir Alex Ferguson ni cha kipekee wakati akiwa kocha wa timu hiyo na ndiyo maana ni vigumu kwa makocha wengine kuvaa viatu vyake,” alisema Jenas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles