24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Jela miaka saba kwa kuchezesha upatu

LEONARD MANG’OHA, DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Jones Moshi na James Gatuni, kulipa faini ya Sh milioni 204 au kwenda jela miaka saba kwa kosa la kuendesha biashara ya upatu na utakatishaji fedha.

Waliohukumiwa ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Rifaro Africa Ltd, Jones Moshi (42) mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam na Mkurugenzi mwenza wa Kampuni hiyo, James Gatuni (35) raia wa Kenya.

Akisoma huko hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, alisema katika kosa la kwanza la utakatoshaji fedha watu kila mmoja anatakiwa kulipa faini ya Sh milioni mbili na endapo watashindwa kufanya hivyo watatakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani.

Mashauri alisema katika shtaka la pili linalohusu utakatishaji fedha haramu kila mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 100 na endapo atashiwa kufanya hivyo atalazimika kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

“Lakini wakishindwa kulipa faini za makosa yote watatakiwa kutumikia kwenda gerezani kama adhabu kwa makosa yote mawili” alisema Mashauri.

Awali Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro, akisaidiana na Wakili Esther Martine na Neema Mbwana alidai mahakamani hapo kuwa wawili hao walitenda kosa hilo kati ya Julai 14 mwaka 2014 na March 31 mwaka 2016, jijini Dar es Salaam na maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kati ya Julai 14 mwaka 2014, na Machi 31, 2016 watuhumiwa waliendesha biashara ya upatu kinyume cha kifungu 171A (1) na (3) cha sheria ya makosa jinai ya mwaka 2002 kana ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2006.

Alisema kati ya Julai 14 mwaka 2014, na Machi 31, 2016 watuhumiwa pia walitenda kosa la kutakatisha fedha haramu kiasi cha Sh bilioni 1.02 kunyume cha ya ya utakatishaji fedha namba 12 ya mwaka 2006 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles