27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Jela miaka 90 kwa kuiba Sh milioni sita

Gavel

Na WALTER MGULUCHUMA- KATAVI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 90 jela baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora zaidi ya Sh milioni sita.

Washtakiwa hao ni mkazi wa Kijiji cha Ilunde wilayani Mlele, Shaban Hamis (35), mkazi wa Kijiji cha Inyonga wilayani Mlele, Masoud Ramadhani (33) na mkazi wa Kijiji cha Kitunda, Ramadhani Agustino (22) na kila mmoja atatumikia miaka 30 jela.

Mwendesha Mashtaka Mkaguzi wa Polisi, Baraka Hongoli, alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Agosti 21, mwaka huu saa nane usiku katika Mtaa wa Uzenga mjini Inyonga wilayani Mlele.

Alidai kuwa washtakiwa hao wakiwa na bunduki aina ya AK 47, walivamia duka la mfanyabiashara, Jonas Davis, kisha wakampora zaidi ya Sh milioni sita.

Aliendelea kudai kuwa washtakiwa hao  walikamatwa Septemba 16, mwaka huu  wakiwa katika nyumba ya wageni iliyopo Mtaa wa Isengo mjini Inyonga wakijiandaa kuwapora fedha wakulima wa tumbaku.

Ilidaiwa kuwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa walikiri kwa maandishi kuwa  walihusika na uporaji huo na wakawaongoza askari polisi hadi kijijini Ilunde na kuonyesha walikoificha AK 47.

Pia washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mengine ya kuvamia nyumba ya mkazi wa Kijiji cha Kalonvya wilayani Mlele, Patrick Nchimbi na kumpora fedha taslimu, vitu vya thamani zikiwemo vocha za muda wa hewani, vitenge na simu za mkononi kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh milioni 3.1 na kumpiga risasi mkononi mke wa mkazi huyo huku Shaban akikabiliwa na kesi nyingine ya kukutwa na bunduki  iliyotengenezwa kienyeji na mtutu wa bunduki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles