27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

JELA MIAKA 30 KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

Na WALTER MGULUCHUMA -KATAVI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi, imemhukumu miaka 30 jela Jackson Eijuel (52), mkazi wa Wakimbiza Katumba, baada ya kukutwa na hatia ya kukamatwa na meno ya tembo manne na vipande vinne sawa na tembo watatu yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 90.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.

Mshtakiwa huyo alipewa uraia wa Tanzania hivi karibuni, baada ya kuishi kwa muda mrefu kama mkimbizi kutoka nchini Burundi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Chiganga alisema kwamba,  mtuhumiwa amethibitika kutenda kosa hilo kinyume cha  kifungu cha sheria namba 235 cha mwenendo wa mashtaka.

Alisema baada ya kusikiliza utetezi wa mshtakiwa,       Mahakama imethibitisha pasi na shaka yoyote kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kukamatwa na meno hayo ya tembo na kumhukumu jela miaka 30.

Awali Mwendesha Mashitaka Mwanasheria wa Serikali,     Fraviani Shiyo, alidai mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa   Jackson Elijuel, alitenda kosa hilo Oktoba 25, mwaka huu,  saa mbili usiku huko katika Kijiji cha Urwila, Tarafa ya Nsimbo, wilayani Mpanda.

Fraviani alidai kwamba, baada ya askari hao kuwa wamepata  taarifa hizo, ndipo walipoandaa mtego na waliweza kumkamata mshtakiwa akiwa na meno manne ya tembo mazima na vipande vinne vyenye uzito wa  kilogramu 27,  yenye thamani ya Sh milioni 99.

Baada ya maelezo hayo, mahakama ilimpa nafasi mshtakiwa ya kujitetea, ambapo aliiomba mahakama imwachie huru, kwani meno hayo ya tembo aliyokamatwa nayo hayakuwa yake, ila yalikuwa ya mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Hussein Samora, ambaye alimtuma kuyabeba kwa kutumia pikipiki yake.

Baada ya utetezi huo, kabla ya Hakimu  kusoma hukumu, Wakili wa Serikali, Fraviani aliitaka mahakama  itoe adhabu kali kwa mshtakiwa, ili iwe fundisho kwa watu wengine  wanaojihusisha na vitendo vya ujangili nchini.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi, Chiganga Ntengwa,   alisema mshtakiwa Jackson amepatikana na hatia kinyume  na kifungu cha sheria namba  235 ya mwenendo wa  mashtaka, hivyo  Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela pamoja na faini ya Sh milioni 99.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles