Upendo Mosha -Siha
MAHAKAMA ya Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, imemhukumu Eliuruma Mushi (25), mkazi wa Kijiji cha Sanya Station kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kufanya shambulio la kingono kwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka tisa.
Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Devota Msofe, alisema hukumu hiyo imetolewa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Alidai kuwa ushahidi ambao ulitolewa mahakamani hapo na mashahidi sita wa upande wa Jamhuri haukuacha shaka yeyote kwamba mtuhumiwa huyo alitenda kosa la unyanyasaji wa kingono kwa mwanafunzi huyo wa Shule ya Msingi Obrain.
Alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha sheria namba 30(1) sura 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na kwamba ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia mbaya ya kutaka kutenda kosa kama hilo katika jamii.
Awali mwendesha mashtaka wa Serikali, Lobulu Mbise alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 6, 2017 majira ya saa 7:30 katika kijiji hicho na baada ya kitendo hicho alitoroka na baadae kukamatwa na polisi.
Alidai kuwa mbali na kufanya shambulio la kingono kwa mwanafunzi huyo, pia alitenda kosa la kumvua nguo mtoto mwingine mwenye umri wa miaka minne na kumshika sehemu zake za siri na kwamba watoto wote hao walikuwa wakiishi na bibi yao kijijini humo.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mwendesha mashtaka huyo aliomba mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine.
mwendesha mashtaka wa Serikali, Lobulu Mbise alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 6, 2017 majira ya saa 7:30 katika kijiji hicho na baada ya kitendo hicho alitoroka na baadae kukamatwa na polisi.