28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Jela miaka 30 kwa kubaka mtoto wa miaka 12

Twalad Salum -Mwanza

MKAZI wa Kijiji cha Buganda, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Bossco Amoni (20), amehukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye miaka 12.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Eric Marley, alitoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili ukiwemo wa mtoto aliyebakwa.

Shahidi wa kwanza alikuwa ni Scholastic Elasto (50) mama wa mtoto huyo ambaye kwenye ushahidi wake  alidai alimzaa Desemba 26 mwaka 2017 na anasoma darasa la tano.

Alidai alipewa taarifa za kuwa mwanaye yuko Kituo cha Polisi Ukiriguru baada ya kukutwa akibakwa.

Naye mtoto huyo kwenye ushahidi wake, alidai alikuwa akienda nyumbani kwao Kijiji cha Ngudama na njiani alikutana na mtuhumiwa ambaye ni shemeji yake.

Alidai mtuhumiwa alimuomba amsindikize dukani kununua wembe na akampitisha njia ya vichakani na alipofika kwenye mti wa mwembe alimbeba na kumlaza chini na kumvua nguo kwa nguvu na kumbaka.

Alidai alipiga kelele kuomba msaada na baada ya muda alipita mzee mmoja akamsaidia.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles