27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Jela miaka 30 kwa kubaka, kumpa mimba mwanafunzi


Na Samwel Mwanga, Maswa


Mahakama ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imemhukumu Domician Faustine (20) mkazi wa mtaa wa Uzunguni mjini Maswa kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na  kumpatia ujauzito mwanafunzi wa kidato cha kwanza(jina linahifadhiwa) wa shule ya Sekondari ya Binza iliyopo wilayani hapa.

Hukumu hiyo imetolewa leo Juni 19, na Hakimu wa mahakama hiyo, Tumaini Marwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.

Hakimu Marwa akisoma hukumu hiyo amesema kuwa anatoa adhabu hiyo kwa mshitakiwa ambaye hakuwepo mahakamani wakati hukumu hiyo ikisomwa kutokana na upande wa mashitaka kuleta mashahidi katika mahakama hiyo ambao walithibitisha kosa la mshitakiwa akiwamo mwanafunzi mwenyewe.

 Amesema kuwa katika Wilaya hiyo vitendo vya wanafunzi  kubakwa na
kupewa ujauzito wakiwa shuleni vimekuwa vikikithiri hali ambayo
imesababisha wanafunzi wengi wa kike wa Shule za Msingi na Sekondari kushindwa kuendelea na masomo.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Nassib Swedy kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba mwaka jana majira ya mchana katika mtaa wa Uzunguni.

Mwendesha mashitaka, Nassib aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa siku ya tukio alimsimamisha mwanafunzi huyo wakati akitoka shuleni kuelekea nyumbanii kwao na kumkamata kwa nguvu na kisha kumwigiza katika moja ya chumba katika nyumba aliyokuwa akiishi mshitakiwa na kuanza kumbaka.

Alisema kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 130 (1) (2) (e) na
kifungu 131(1) vifungu vya  sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16
marejeo ya mwaka 2002.

Kwa kuwa mshitakiwa hakuwepo wakati hukumu yake ikisomwa mahakama iliamuru mshitakiwa atafutwe na mdhamini wake na akikamatwa aanze kutumikia kifungo chake mara moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles