22.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Jela miaka 30 kwa dawa za kulevya

Na KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi imemtia hatiani na kumuhukumu kwenda jela miaka 30 mfanyabiashara Shaban Kalikuta kwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Mshtakiwa huyo alitiwa hatiani mbele ya Jaji Lilian Mashaka baada ya Mahakama kujiridhisha kwamba Jamhuri imethibitisha kosa bila kuacha shaka.

Mshtakiwa alikamatwa Agosti 29 mwaka 2001 katika mtaa wa ufipa Kinondoni Dar es Salaam akiwa na dawa za kulevya gram 238.24 aina ya heroin hydrochloride. 

Upande wa Jamuhuri ulikuwa na mashahidi 8 na vielelezo 5 ili kuthibitisha kesi. 

Baada ya kuchambua ushahidi kwa ujumla wake mahakama imeona kwamba  upande wa  Jamhuri umethibitisha kesi bila kuacha shaka.

Jaji Mashaka alimtia hatiani mshtakiwa  na kumuhukumu kwenda jela miaka 30.  

Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Costantine Kakula na Batilda Mushi na kwa upande wa utetezi uliwakilishwa na Wakili Abraham Senguji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,647FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles