29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Jela miaka 12 kwa kutorosha binti

 KHAMIS SHARIF-UNGUJA

MAHAKAMA ya Mkoa Vuga mjini Unguja, imemuhukumu kifungo cha kwenda jela miaka 12, Abuu Khamis Ibrahim (40) mkaazi wa Meya Mjini Unguja kwa kosa la kubaka, kulawiti na kumtorosha mtoto wa kike miaka 15 ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mshtakiwa alipewa adhabu hiyo na mahakama hiyo, baada ya kutenda kosa hilo Febuari 24, mwaka jana kinyume na sheria.

Akisomewa shtaka na Hakimu wa Mahakama hiyo, wiki iliyopita, Salum Hassan Bakari na Mwendesha Mashtaka, Shamsi Yassin alisema mshtakiwa alimtorosha mtoto huyo ambaye yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake na kumfanyia udhalilishaki ambao ni kinyume na haki za binadamu.

“Febuari 24, mshtakiwa alimtorosha mtoto ambaye yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake na kuondoka naye saa 10 jioni na kumrejesha saa 3 usiku na kufanyia vitendo vya udhalishaji kwa kumbaka na kumlawiti,”alisema hakimu Bakari Alisema mshtakiwa, alipewa adhabu ya kifungo cha miaka 12 jela na kutoa fidia ya Sh milioni moja.Kesi hiyo, ilianzwa kusikilizwa mahakamani hapo Julai 7, mwaka jana ambapo mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa.

Katika hatua nyingine za kupambana na vitendo hivyo,kesi 42 za matukio ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto, zimeripotiwa katika dawati la jinsia Mkoa wa Kaskazini Unguja Januari hadi Mei, mwaka huu.

Akiwasilisha ripoti juu ya matukio hayo, Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Kaskazini Unguja, Fatma Juma Mahmoud alisema matukio hayo yamefanyika wilaya za Kaskazini ‘A’ matukio 19, huku Kaskazini ‘B’ matukio 23.

Alisema idadi kubwa ya kesi hizo , zipo ngazi ya upelelezi hadi sasa kwa lengo la kubaini ukweli juu ya watu wanaotuhimiwa kufanya matukio hayo.

Alisema kesi nyingine mbili zipo ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), zikisubiri kufikishwa mahakamani.

Akitoa muelekeo wa kesi ambayo ipo mahakamani hadi sasa, alisema ni kesi moja na kwamba kesi hiyo imesita kuendelea kuskilizwa kwa kile alichodai uwapo wa ugonjwa wa corona.

Ofisa Dawati la Jinsia Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, Khamis Kona Khamis alisema kuendelea kuwepo kwa matukio hayo katika wilaya na mkoa huo, kunachangiwa na sababu mbali mbali ikiwemo ucheleweshaji wa uandaaji wa kesi kabla kufikishwa Mahakamani.

Huku Mratibu wa Dawati la Jinsia Mkoa huo, Suleiman Juma, alisema jeshi la Polisi wanakabiliana na hali ngumu katika mapambano hayo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles