28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

JELA MAISHA KWA KUMBAKA MJUKUU WAKE

Na MURUGWA THOMAS – NZEGA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu kifungo cha maisha Hubasha Ngasa (62) mkazi wa Kijiji cha Ngonho baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka minne.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Serafina Nsana, alisema adhabu hiyo imetolewa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliowasilisishwa na upande wa mashtaka.

Awali Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Polisi, Melito Ukongoji, aliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa la kumbaka mtoto huyo Aprili 24, mwaka 2016 baada ya kuachwa na wazazi wake walipokwenda kulima.

“Baada ya muda wazazi wa mtoto huyo  wakiwa shambani walisikia kelele za mtoto na walipokwenda kuangalia nini kimetokea,  walikuta tayari mshtakiwa  amembaka na kumjeruhi sehemu zake za siri,” alidai Ukongoji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles