28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

JE, UNAMKUMBUKA MTOTO HUYU ALIYEISHTUA DUNIA KWA KUVUTA SIGARA 40 KWA SIKU?

MWAKA 2010 akiwa na umri wa miaka miwili tu aliishtua dunia pale alipoonekana katika picha na video zilizosambazwa mitandaoni akivuta sigara mfululizo.

Miaka miwili baadaye aliweza kubadilika na kuachana na tabia hiyo, lakini akaibuka na tatizo lingine la ulaji holela lililomfanya anenepeane kabla ya sasa kuweza kulidhibiti.

Mvulana huyu ambaye sasa ana umri wa miaka saba, Aldi Rizal alikuwa gumzo la vyombo vya habari duniani wakati alipogundulika katika kijiji masikini kule Sumatra, Indonesia.

Ni baada ya kuonekana akivuta sigara na wingu zito la moshi wake limemzunguka huku akiendesha baiskeli yake ya magurudumu matatu.

Mbaya zaidi picha nyingine ya video ilimuonesha akivuta sigara moja baada ya nyingine huku familia yake ikimtazama tu na hilo lilisababisha wengi kusafiri umbali wa maili nyingi kwenda kumuona.

Kelele zilizopigwa duniani ziliifanya Serikali ya Indonesa kuzindua kampeni ya kukabiliana na tatizo la watoto wanaovuta sigara na kuendesha programu maalumu ya matibabu kumsaidia Aldi kuachana na tabia hiyo.

Inadhaniwa kwamba theluthi moja ya watoto wote nchini Indonesia hujaribu kuvuta sigara kabla hawajafikisha umri wa miaka 10.

Hilo kwa mujibu ya wachambuzi wa mambo linatokana na serikali kushindwa kuwalinda, kudhibiti matangazo holela yanayochochea uvutaji sigara pamoja na uvutaji sigara kuonekana sehemu ya utamaduni wa taifa hilo.

Aldi alichukuliwa kupelekwa kuhudhuria tiba kwenye mji mkuu wa Jakarta kwa wiki mbili ili kumweka mbali na tabia yake ya kuvuta sigara 40 kwa siku na kujifunza kuwa mtoto wa kawaida kwa mara ya kwanza.

Wakati wa tiba yake, Aldi alionana na wataalamu wa watoto ambao walimtia moyo mama yake kumfanya mtoto wake awe bize na michezo na kumfundisha kuhusu athari ya kuvuta sigara.

Mmoja wapo – Dr Kak Seto – bado anaendelea kuonana na Aldi na familia yake mara kwa mara kuhakikisha harudii tena katika tabia yake hiyo ya zamani.

Mama yake, Diane Rizal (30), alisema: kuna watu wengi ambao bado humpatia Aldi ofa ya sigara, lakini mvulana huyo huwakatalia akisema atakuwa na huzuni iwapo ataanza tena kuvuta sigara na kuumwa umwa.

Awali wakati tulipoanza juhudi za kumwachisha Aldi sigara, alijikuta ‘akiugua’ kwa kuzikosa sigara, wakati akihaha kuzoea hali hiyo mpya na nilimwita Dk. Seto kwa msaada.

“Kufikia mwaka 2014 alikuwa akipunguza kiwango cha sigara kutoka 40 hadi tano kwa siku kabla ya kuacha kabisa.”

Hata hivyo, Rizal akaja baadaye kuwa na wasiwasi na uzito wa mwanae, kwa vile baada ya kuacha kuvuta sigara akaja na tabia ya kupenda ulaji kiholela.

Rizal alisema kwamba mvulana huyo alikuwa akiomba chakula kwa namna ile ile aliyokuwa akiomba sigara kabla hajaacha na familia ilikuwa ikihaha kumridhisha.

Rizal alisema awali Aldi alipoacha sigara alikuwa akidai wanasesere wengi mara huyu mara yule.

 

“Angepigisha kichwa chake ukutani iwapo asingepata kile anachotaka. Ni kwa sababu tulimpatia sigara, kwa sababu ya hasira zake na uliaji liaji wake.

'Sasa simpatii sigara, lakini anakula sana. Kwa uwapo wa watu wengi wanaopishi nyumbani ni vigumu kumzuia asipate chakula,” anasema mama yake.

Aldi pia humsaidia mama na baba yake Mohamed katika genge lao sokoni, ambako umbo lake kubwa pamoja na uso wake mviringo uliotuna huvutia macho ya wengi.

“Nina furaha wakati watu wanapotaka kuzungumza naye kwa sababu wanamfahamu,” anakiri Rizal.

“Lakini huudhika wakati wanapomzungumzia kama mtoto mvuta sigara. Inanifanya nijihisi kana kwamba wananituhumu kwa kuwa mzazi mbaya.”

Bwana na Bibi Rizal waliamua kumpeleka Aldi kwa mtalaamu wa mlo kumchunguza, ambako alipewa ushauri wa namna ya kupangilia mlo ili apunguze uzito wake.

“Aldi alikuwa na uzito mno usioendana na umri wake,” alisema mtaalamu wa mlo, Fransisca Dewi. “Uzito unaomstahili ni kilo 17 hadi 19 lakini ana uzito wa kilo 24 sasa.”

Kwa sababu ya kuachana na tabia mbaya ya uvutaji wa sigara na kurukia ile ya ulafi pengine vyakula holela na athari za uvutaji sigara katika umri mdogo uliathiri homini, insulin na kiwango cha glucose katika mwili wa binadamu.

Sasa, Aldi amerudi nyumbani katika kijiji chake cha uvuvi na yu katika upangiliaji wa mlo hasa mbogamboga na matunda pamoja na kiwango kidogo cha vyakula avipendavyo.

Rizal huwalazimisha nduguze Aldi na familia nzima kutompatia vyakua holela wakati asipokuwepo nyumbani. Mkakati huo umefanikisha upunguzaji wa uzito.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,900FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles