22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

JE MBELGIJI AUSSEMS ATAIPA SIMBA MAFANIKIO GANI?

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM


UJIO wa makocha wapya katika klabu za Tanzania imekuwa ni jambo la kawaida, tayari wimbo wa timu ajiri mwingine umeshika na kunasa katika akili za wadau na wapenda soka.

Yanga, Simba na Azam ni klabu pendwa ambazo ndiyo zinazoongoza kwa dhahama hii ya kufukuza na kuajiri kila kukicha.

Klabu hizi zenye umaarufu Afrika Mashariki na Kati , zimekuwa zikitumia matokeo mabovu, mwenendo ovyo wa timu kuwatimua makocha na kuwapa mikataba  mipya wengine.

Siku  nne zilizopita imshuhudiwa klabu ya Simba ikiingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha wake mpya raia wa Ubeligiji, Partick Aussems.

Simba ambao msimu uliopita walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuukosa kwa kipindi cha miaka sita , wataonekana msimu ujao chini ya kocha huyo, ambaye alifanyiwa mahojiano saa tano, kabla ya kupewa mkataba.

Aussems ambaye aliwapiku makocha takribani 55, amepewa jukumu la kuhakikisha Simba inakuwa klabu bora Afrika, ikiwa ni pamoja na kutetea taji la Ligi Kuu msimu ujao.

Makocha waliofundisha Simba kuanzia mwaka 2003 hadi sasa na kuipa mafanikio klabu hiyo ni Mkenya, James Siang’a (2003-2004), Mwafrika Kusini,  Trott Moloto  (2005), Patrick Phiri- Zambia (2005), Mbrazil Neidor dos Santos (2006), ,Talib Hilal (2007)  na Mserbia Milovan Curkovic (Novemba 2007-April 2008), Krasmir Benzinsik  (Mei 2008- 2009).

Mzambia Patrick Phiri (2009-2010), Mbulgaria  Krasmir Benziski (2011), Mganda Moses Basena (2011), Curkovic (201/ 12), Mfaransa Patrick Liewig, (Desemba 2012-Mei 2013) na Abdallah  Kibadeni (Juni 2013-Novemba).

Mcroatia  Zdravko Logarusic (Desemba 2013-Juni 2014), Phiri (Agosti 2014-Novemba 2014), Msebia  Goran Kopunovic (Desemba 2014 -Juni2015), Mwingereza Dylan Kerr (Julai 2015- Januari 2016), Jackson Mayanja (Januari 2016 –Mei).

Joseph Omog Februari 2016 hadi Desemba 2018, (Pierre Lenchatre (Desemba 2017-  Juni 2018) na Mbelgiji, Patrick Aussems (Julai mwaka huu).

Kati ya makocha hao, Siang’a aliiwezesha klabu hiyo, kufika robo fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003.

Makocha  wengine alioipa mafanikio Simba kwa kutwaa  ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania  ni pamoja na Siang’a ( 2003) Hilal mwaka 2007, Phiri (2009/10), Curkovic (2011/12) na  Lenchatre (2017/18).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles