Jay-Z, Meek Mill wasaidia wafungwa kujikinga Corona

0
779

New York, Marekani

WAKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Jay-Z na Meek Mill, mwishoni mwa wiki iliopita walitoa msaada kwa wafungwa wa vifaa vya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.

Vifaa hivyo vya kuvaa mdomoni vilikuwa 100,000 na vilisambazwa sehemu mbalimbali za magereza ambako kunadaiwa kuwa na msongamano mkubwa.

Watu wametakiwa kupunguza misongamono, lakini kwa wafungwa inaonekana kuwa ngumu jambo ambalo wawili hao wameguswa na kuamua kusaidia.

Siku chache zilizopita Jay Z na Rihanna waliungana pamoja na kutoa kiasi cha dola milioni 2 ambazo ni zaidi ya bilioni 4 kwa ajili ya kusaidia chakula hasa kwa watu wenye uhitaji katika kipindi hiki kigumu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here