28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

JAY Z ATUMIA BIL. 264/- KUNUNUA NYUMBA YA WATOTO WAKE

CALIFORNIA, MAREKANI


UPENDO wa familia ni watoto na wakati wote wanapopatikana, wazazi huwa na furaha kwa kuwaandalia sehemu nzuri, huku wakiwekewa mipango kadha wa kadha kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Mkali wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Shawn Carter ‘Jay-Z’ na mke wake, Beyonce, wameonyesha namna wanavyoandaa maisha bora ya watoto wao mapacha wanaowatarajia hivi karibuni.

Wakali hao wa muziki duniani wametumia dola milioni 120, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 264 za Kitanzania kununua nyumba kwa ajili ya watoto hao mapacha wawili.

Wapenzi hao, ambao ndoa yao ina mvuto mkubwa na mfano wa kuigwa na mastaa wengi duniani, wametumia kiasi hicho cha fedha kuwanunulia nyumba yao ili watoto hao wakizaliwa waikute.

Eneo la nyumba hiyo lina ukubwa wa eka mbili na linalindwa na ulinzi mkali kwa ajili ya usalama wa mali zilizopo ndani ya eneo hilo.

Inasemekana kuwa, madirisha ya nyumba hiyo yamefungwa vifaa maalumu kwa ajili ya kuzuia kushambuliwa na risasi.

Nyumba hiyo ina jumla ya vyumba 11 vya kulala, pamoja na sehemu ya kupaki magari 15, chumba cha kutayarishia muziki na sehemu nne za wazi za kuogea (swimming pool).

Naye mwanamitindo maarufu nchini Hispania, Georgina Rodriquez, ambaye ni mchumba wa mshambuliaji wa klabu ya soka ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, anatarajia kujifungua mapacha.

Gazeti la The Sun liliripoti kwamba, mchezaji huyo aliandaa nyumba yenye thamani ya Sh bilioni 13 kwa ajili ya kufikia watoto wake hao mapacha na katika nyumba hiyo aliweka vito mbalimbali vya thamani kwa ajili yao.

Ronaldo, ambaye kwa sasa ana mtoto mmoja wa kiume anayejulikana kwa jina la Cristiano Jr, ujio wa watoto hao utaongeza ukubwa wa familia yake, lakini kwa mchumba wake huyo mwenye umri wa miaka 23, itakuwa ndiyo watoto wake wa kwanza.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,900FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles