26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 16, 2021

JAY-Z AKUTANA NA LUKAKU

 

NEW JERSEY, MAREKANI


RAPA Jay Z, mapema wiki hii alikutana na staa wa soka anayekipiga katika klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku, mara baada ya kumalizika kwa shoo yake ya ‘On the Run II Tour.’

Lukaku alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti picha mbili, moja akiwa na Jay Z na nyingine akiwa na mwanachama wa Roc Nation, DJ Khaled, kisha mchezaji huyo kuandika kuwa ndoto zake zimekamilika kukutana na mastaa hao wa muziki duniani.

Hata hivyo, Jay Z naye aliandika kwenye ukurasa wa Instagram kupitia picha hiyo iliyowekwa na Lukaku, huku akisema: “Nitakuona tena hivi karibuni, endelea kupambana tutaongea zaidi.”

Lukaku ni mchezaji wa kwanza katika Ligi ya England kuingia kwenye uongozi wa Roc Nation ambayo ipo chini ya Jay Z. Kampuni hiyo ya muziki imewasainisha wanamichezo mbalimbali wa soka na mpira wa kikapu kwa ajili ya kuzidi kuitangaza, miongoni mwao ni Jerome Boateng wa Bayern Munich na Kevin Durant wa kikapu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
161,841FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles