26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

JAY-Z ‘AFOKEWA’ NA WANAWE

LOS ANGELES, MAREKANI


MKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Jay-Z, amesema mwanawe Blue Ivy, amekua kwa sasa baada ya mtoto huyo kufoka kutokana na kuchukizwa na baadhi ya mambo anayoyafanya baba yake.

Blue Ivy ambaye ni mtoto wa kwanza wa Jay Z mwenye umri wa miaka sita, mwishoni mwa wiki iliyopita alimfokea baba yake kutokana na kauli yake ya kumtaka aingie kwenye gari.

Jay Z amesema muda ulikuwa umefika wa kumpeleka shule mwanawe, hivyo alimwambia aingie kwenye gari kwa safari, hata hivyo Jay Z alichelewa kuingia wakati huo mtoto tayari alikuwa ameingia.

Wakiwa wanaelekea shule, Blue Ivy, alimwambia baba yake: “Baba ujue nachukia sana jinsi unavyoniambia niingie kwenye gari, jinsi unavyotamka kauli yako nachukia sana,” Blue Ivy alimwambia Jay Z.

Msanii huyo amedai anaamini mtoto wake amekuwa kwa kuwa mara kwa mara amekuwa akimuuliza maswali mbalimbali kama mtu mwenye umri mkubwa.

“Mwanangu amekuwa, amekuwa na maswali kila kukicha na mwishoni mwa wiki iliyopita alionesha kunifokea kutokana na kuchukizwa na baadhi ya vitu ninavyovifanya,” alisema Jay Z.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles