Jay Dee awashangaa wasanii kwa lawama zao

0
719

GLORY MLAY

MSANII mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ amesema wasanii wengi wanakosea kutoa lawama kwenye vyombo vya habari kutokana na kazi zao kutofanya vizuri.

Lady Jay Dee amesema, msanii bila juhudi zake hawezi kufanikiwa wala kufikia malengo ambayo amejiwekea, hivyo hakuna sababu ya kuvilaumu vyombo vya habari.

“Wasanii wanajua kutoa lawama kwamba kazi zao hazipigwi redioni au kwenye runinga, lakini wanatakiwa kutambua ubora wa kazi hizo pengine kazi wanazotoa hazina kiwango na wala hazina mvuto wa kusikilizwa.

“Hivyo wapunguze lawama na wafanye kazi kwa bidii ninaamini watafikia malengo yao na kazi zao zitakwenda mbali zaidi,”alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here