JASON DERULO KUTUA KENYA WIKI HII

0
652

NAIROBI, KENYA


MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Jason Desrouleaux ‘Jason Derulo’, anatarajia kuwasili nchini Kenya wiki hii kwa ajili ya uzinduzi wa Coke studio Africa awamu ya tano.

Derulo ambaye anatamba na wimbo wake wa ‘Swalla’, ameandaliwa maprodyuza wawili mmoja kutoka Nigeria, Masterkraft na DJ Maphorisa wa Afrika Kusini.

Hata hivyo, prodyuza hao watafanya kazi ya kuwaandalia midundo wasanii kutoka nchi zaidi ya 30 za Afrika ambazo ni Afrika Kusini, Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Ivory Coast, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, DRC na Cameroon.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here