NYOTA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Jason Derulo, ameomba msamaha kwa mashabiki wake wa Afrika Kusini mara baada ya kutamka maneno yaliyotafsiriwa kuwa ni dharau kwa waliohudhuria onyesho lake.
Mkali huyo aliwauliza mashabiki wake kama wanajua Kiingereza ‘Y, all speak English, right?’ , maneno yaliyozua vurugu kwenye onyesho hilo lililoambatana na utolewaji wa tuzo za Afrika Kusini maarufu kama ANN7 zilizofanyika usiku wa jana huko Johannesburg.
“Sikujua kama naweza kusababisha fujo kiasi kile sababu yale ni maneno ya kawaida tu, nalazimika kuwaomba radhi mashabiki wangu wa ndani na nje ya Afrika Kusini kwa tukio lile,” alisema Derulo.