21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

JASON DERULO AJIUNGA GLOBAL CRYPTO

TORONTO, CANADA

MTANDAO wa Global Crypto (GCOX), umethibitisha kumsainisha mkali wa muziki nchini Marekani, Jason Derulo, kuwa mmoja kati ya mastaa ambao wanatambulika na mfumo mpya wa mastaa wenye mashabiki wengi duniani.

Msanii huyo ambaye amefanya vizuri kwa kipindi cha hivi karibuni kutokana na wimbo wake mpya wa ‘Colors’ uliotumika kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, anaungana na mastaa wengine kama vile mchezaji wa zamani wa Liverpool na Real Madrid, Michael Owen.

Msanii huyo ametajwa kuwa miongoni mwa wasanii waliofanya mauzo ya kopi zaidi ya milioni 30 katika nyimbo zake kama vile Wiggle, Talk Dirty, In My Head na Whatcha Say.

“Kila kitu kimekwenda sawa kati yangu na uongozi wa GCOX, nina furaha kuwa mmoja kati ya watu ambao wanaingia kwenye mfumo huo mpya,” aliandika msanii huyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles