23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JARIBIO LA RAIS TRUMP LAGONGA MWAMBA

Washighton, Marekani


MAHAKAMA ya Jimbo la Hawaii, imezuia utekelezaji wa marufuku mpya wa usafiri iliyokuwa imetangazwa na Rais, Donald Trump.

Marufuku hiyo ilizuiwa saa chache kabla ya kuanza kutekelezwa saa sita usiku Alhamisi.

Jaji Derrick Watson alisema ushahidi uliotolewa na Serikali katika kutetea marufuku huo ni wa kutiliwa shaka.

Serikali ilikuwa imejitetea mahakamani ikisema marufuku hiyo inalenga kuimarisha usalama wa taifa.

Rais Trump ameeleza uamuzi huo wa jaji kuwa wa kushangaza na akasema mahakama imevuka mpaka.

Agizo lililokuwa limetolewa na Trump ambalo lilifaa kuanza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo, ungepiga marufuku kwa miezi mitatu raia kutoka nchi sita zenye Waislamu wengi kuzuru Marekani.

Mataifa hayo ni Iran, Libya, Syria, Somalia, Sudan na Yemen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles