29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

JARIBIO LA KOMBORA KOREA KASKAZINI LASHINDWA

SEOUL, KOREA KUSINI


JARIBIO jipya la Korea Kaskazini kurusha kombora limeshindikana baada ya kuripuka muda mfupi tu lilipofyatuliwa jana, ikiwa ni  siku moja tangu ilipoonesha hazina yake ya makombora katika gwaride kubwa la kijeshi.

Kushindwa  huko , ambako  kunaonekana  kwa  umma  kama  kitu cha  fadhaa  kwa  serikali  ya  nchi  hiyo, kumekuja  huku  hali  ya wasi  wasi  ikiongezeka   katika  rasi ya Korea kuhusu  dhamira ya  taifa hilo kujipatia  silaha  za  nyuklia.

Hata  hivyo  haikuwezekana  kufahamika mara  moja  aina gani  ya  kombora hilo.

Jaribio  hilo  limekuja baada  ya  Korea  Kaskazini  kuonesha karibu  makombora 60  ikiwamo jipya lenye uwezo wa kuvuka  mabara wakati wa  gwaride siku  ya  Jumamosi  kuadhimisha  miaka  105 ya  kuzaliwa  kwa mwasisi  wa  taifa  hilo,  Kim II-Sung.

Sherehe  hizo zilifanyika  mbele ya kamera za mashirika  ya habari duniani  yaliyoalikwa na ambayo  yalikuwapo pia wakati wa jaribio  la  kurusha  kombora  hilo  lililoshindwa.

Aidha kushindwa  kwa kombora  hilo  kunakuja  saa chache  kabla  ya ziara  ya  Makamu  wa  Rais  wa  Marekani,  Mike  Pence  nchini hapa,  ambako  suala la Korea Kaskazini  litakuwa  ajenda  ya  juu.

Korea  Kaskazini  ina  tabia  ya  kurusha  makombora  kuadhimisha sherehe  muhimu  za  kisiasa, ama  kama  ishara  ya  ukaidi  wakati  maafisa  wa  ngazi  ya  juu  wa  Marekani  wanapofanya ziara  eneo  hilo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles