33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Japan yajenga vyoo vinavyoonesha kinachoendelea ndani

MOJA ya maeneo maarufu nchini Japan imeongeza kivutio kisicho cha kawaida ambacho ni vyoo vya umma angavu.

Mbunifu wa vyoo hivyo ambaye pia ni Mhandisi Shigeru Ban, alisema vyoo hivyo ambavyo unaweza kuona mwenzio anachofanya upande wa pili au akiwa ndani vimewekwa kwenye Mji wa Shibuya wenye watu wengi.

Ingawa hilo linaonekana kama kuvuka mipaka ya utamaduni, lengo ni kubadilisha mitazamo ya watu kuhusu vyoo vya umma.

Mbunifu Shigeru ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Pritzker anasema: “Vyoo angavu vimewekwa katika bustani mbili za Shibuya, ya – Yoyogi Fukamachi na Haru-no-Ogawa.

“Kuna mawili yanayotutia wasiwasi, wakati unaingia choo cha umma, hasa vilivyo maeneo ya bustani,” anasema kwenye tovuti rasmi ya mradi huo na kuongeza: “Kwanza ni usafi, pili ni ikiwa kuna mtu ndani au la.”

Ubunifu wa Shigeru Ban unatoa ufumbuzi wa matatizo hayo mawili baada ya utengenezaji wake wa vyoo ambavyo ukuta wake ni kioo – kwanza mtu anaweza kuona kinachoendelea ndani akiwa nje.

“Hili linamruhusu mtu kuangalia kama choo ni kisafi na iwapo kuna mtu anayekitumia,” inasema taarifa hiyo. Inaongeza: “Usiku, vyoo hivyo vinatoa mwanga wa kuvutia kama taa ya kandili.”

Inakuaje unapovitumia?

Vyoo hivyo vina mwonekano wa kuvutia na rangi za kupendeza.

Kinachofurahisha zaidi ni kwamba unaweza kusema ikiwa kioo kimeganda kwa barafu au la. Kuta zake zimewekwa kioo na kumfanya mtumiaji kuwa na hisia kwamba anaonekana anachofanya kwa nje.

Lakini mtu anapoingia ndani na kufunga mlango vioo vinabadilika na kutanda wingu fulani ili kumpa faragha.

Hivyo basi, ni muhimu mtu kufunga mlango – sehemu iliyo chini ya mpini wa kufungia vinginevyo, kwa nje watu watakuwa wanajionea maajabu yaani kila kitu kinachoendelea.

Nchini Japan, kuna dhana kwamba vyoo vya umma ni vichafu na ubunifu huu unajitahidi kukabiliana na dhana hiyo

Katika bustani zote mbili kuna choo wa wanawake, wanaume na kile cha watu wenye ulemavu.

“Utumiaji wa vyoo vya umma Japan ni mchache kwa sababu ya dhana kwamba ni vichafu, vina giza, vinanuka na kuogopesha.”

Ili kuondoa dhana hiyo, mji umeamua kubadilisha vyoo 17 vilivyopo miji ya Shibuya na Tokyo.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles