25.7 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Jangili apewa adhabu ya kuangalia filamu ya wanyama

Na MWANDISHI WETU

JANGILI mmoja nchini Marekani amepewa adhabu ya kuangalia filamu ya wanyama ya Bambi kila mwezi baada ya kukutwa na hatia ya kuua mamia ya mbawala.

Mwindaji huyo kutoka Missouri, David Berry Jr, anatakiwa kuangalia filamu hiyo mara moja kwa mwezi wakati akitumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Alikamatwa Agosti mwaka jana, pamoja na ndugu zake wawili kwa kosa la kuwaua mbawala, kisha kuwachinja na kuondoka na vichwa huku akiacha miili ya wanyama hao ikioza.

Kesi hiyo ni moja ya kesi kubwa zaidi za ujangili kuwahi kuripotiwa kwenye historia ya Jimbo la Missouri.

Pamoja kuhukumiwa kwenda jela kwa kukutwa na hatia ya kuwinda mbawala kinyume cha sheria, Jaji Robert George alimwamuru Berry Jr kuangalia filamu iliyoandaliwa na Kampuni ya Walt Disney inayoitwa Bambi.

Alitakiwa kuiangalia kwa mara ya kwanza kabla Desemba 23 mwaka jana, na baada ya hapo kuangalia walau mara moja kila mwezi katika kipindi chote atakachokaa jela.

Filamu hiyo ya katuni ya mwaka 1942 inaangazia maisha ya familia moja ya mbawala waliolazimika kuishi bila mama yao baada ya kuuawa na majangili.

Gazeti la the Springfield News-Leader lilisema kuwa uchunguzi wa miezi kadhaa uliofanyika kwenye majimbo mbalimbali ulisababisha kunaswa kwa Berry Jr, baba yake David Berry Sr na kaka yake Kyle Berry.

Japo idadi kamili ya mbawala waliouawa haijajulikani, mhifadhi wa Kaunti ya Lawrence Andy Barnes alisema inaweza kufikia mamia.

Berry Jr alipewa adhabu ya kwenda jela baada ya kukiri mashtaka yalikuwa yanamkabili.

Pia alipewa adhabu ya kwenda jela siku 120 kwa kukiuka masharti ya dhamana yake ya matumizi ya silaha za moto.

Kamisheni ya Uhifadhi ya Missouri aliwafutia vibali vya uwindaji jangili huyo na baba yake.

Imeandaliwa kwa msaada wa BBC

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,897FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles