26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

JANET JACKSON: NIKO TAYARI KWA ZIARA YA MUZIKI

NEW YORK, MAREKANI


BAADA ya kukaa nje ya muziki kwa muda mrefu kutokana na mipango ya uzazi, msanii Janet Jackson, amewaambia mashabiki wake kwamba kwa sasa yuko tayari kurudi kwenye kazi yake ya muziki.

Mapema mwaka jana msanii huyo alitangaza kupumzika kazi ya muziki huku akipanga kuongeza familia akiwa na alioyekuwa mume wake, Wissam Al Mana, hatimaye wakafanikiwa kupata mtoto Januari mwaka huu lakini kwa sasa wameachana.

Baada ya kuachana kwao mwanamuziki huyo amesema wakati wa kurudi katika kazi yake ya muziki ambayo imempa mafanikio makubwa ndiyo huu sasa.

“Nataka kuwa muwazi kwenu mashabiki wangu, ni kweli nimeachana na baba wa mtoto wangu na sasa shauri lipo mahakamani na namwachia Mungu. Nawashukuru wote ambao walikuwa pamoja nami kwa kipindi chote na sasa nawaambia kuwa nipo tayari kurudi kwenye muziki kama nilivyosema awali kabla ya kufanya mapumziko, ninahitaji sapoti yenu katika ziara yangu mpya,” alisema Janet.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles