25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Janet Jackson na ndoto za jina la Michael Jackson

michael-and-janet-jackson-at-the-1993-grammys-308138BADI MCHOMOLO NA MITANDAO

WAHENGA walisema jina huumba, ndivyo ilivyo kwa msanii maarufu nchini Marekani, Janet Jackson (50), ambaye kwa sasa anatarajia kumpata mtoto wa kiume, huku akiwa ameshachagua jina la Michael kuwa ndilo la mtoto wake atakayezaliwa wakati wowote kutoka sasa.

Miaka saba sasa imetimia tangu Michael Jackson, mfalme wa muziki wa Pop aliyevunja rekodi ya mauzo ya albamu yake ya ‘Thriller’ mwaka 1982, ambaye ni kaka wa Janet, afariki dunia.

Licha ya kuanza maandalizi ya kununua mavazi kwa ajili ya mtoto wake huyo na mume wake, Wissam Al Mana, imani yake ni kwamba jina hilo licha ya kuwa kumbukumbu kubwa ya kaka yake, lakini pia litaleta mafanikio na upendo mkubwa kati ya mtoto huyo, familia yake na maisha yake kwa ujumla.

Michael na Janet wamezaliwa katika familia ya watoto 11, huku Michael akiwa wa nane kati ya 11 na kati ya watoto hao, Michael alikuwa akimpenda sana Janet, aliyezaliwa miaka nane baada ya kuzaliwa kwake.

Watoto 10 kati ya 11 walizaliwa na mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Katherine Esther Scruse. Mwaka 1995 Janet na Michael walitoa wimbo wa ‘Childhood’ na walikuwa wakibadilishana hadi nguo kutokana na kukaribiana kimaumbo.

Baada ya Juni 25, 2009 kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani, Janet na kaka yake walikuwa wameonana katika sherehe ya familia ambapo walipanga mipango mingi ya kimuziki, lakini haikukamilika kutokana na kifo cha Michael.

Wakati wa kifo chake, Janet hakuwa akitazama runinga, pia aligoma kufanya mahojiano kuhusu kifo hicho kutokana na uchungu aliokuwa nao. Michael alifariki akiacha watoto watatu, na sasa Janet ndiye anatarajia kupata mtoto wa kwanza akiwa na miaka 50.

Hivyo kutokana na upendo huo kwa marehemu kaka yake, ameona bora jina hilo ampe mtoto wake mtarajiwa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles