29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

JANET JACKSON ATAKAVYONUFAIKA KUVUNJIKA NDOA YAKE

NEW YORK, MAREKANI


 MSANII wa muziki wa Pop nchini Marekani,, mwenye miaka 50, anatarajia kuingiza kiasi kikubwa cha fedha baada ya kuachana na mume wake tajiri kutoka Qatar, Wissam Al Mana.

Janet amethibitisha kuachana na mume huyo kwa madai kwamba, tajiri huyo hana mapenzi ya dhati na amekuwa akiibagua familia yake.

Wissam Al Mana ni mfanyabiashara mkubwa duniani anayemiliki kampuni kubwa zaidi ya 55, kuvunjika kwa ndoa yake kunadaiwa kutampa utajiri mkubwa Janet, atakayekuwa kimlea mtoto wao mmoja wa kiume aliyezaliwa Januari, mwaka huu.

Wissam Al Mana anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya pauni milioni 800, zaidi ya Sh trilioni mbili za Tanzania.

Hata hivyo, sheria za Marekani ni kwamba wanandoa wakiachana wanatakiwa kugawana mali, hivyo kutokana na hali hiyo, Janet anaweza kupata zaidi ya Sh trilioni moja, ikiwa ni sehemu ya mgawo wa kuachana kwao pamoja na kiasi kingine cha huduma kwa mtoto wao.

Kitendo hicho ndicho kinachowafanya wasanii matajiri nchini Marekani kuchelewa kufanya maamuzi ya kufunga ndoa, wakiogopa kugawana mali watakapoachana.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Janet inaeleza kwamba, msanii huyo alilenga kudumu kwenye ndoa kutokana na umri wake mkubwa na hakufuata fedha kwa kuwa naye ana utajiri wa zaidi ya dola milioni 150 za Marekani, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 331 za Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles