26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Jamii yatakiwa kuwafundisha watoto malezi bora

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

SHEIKHE wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu ameitaka jamii kujikita kufundisha malezi bora kwa watoto na vijana ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata elimu.

Akizungumza katika mahafali ya nne ya Shule ya Sekondari Ororimu ya wilayani Kondoa mkoani Dodoma, Sheikhe Rajabu amesema jamii ina wajibu wa kuhakikisha inatoa malezi bora kwa watoto na vijana ili siku za baadae wawe na maadili mema.

“Tusiwe wafugaji tuwe walezi waweza ukampa mtu kila kitu lakini wewe ni sawa na wafugaji wengine tujikite katika malezi hasa malezi bora na hapa malezi yameonekana hapa Ororimu kwani kuna ubora ambao umeonekana sasa ni wakati wa kujitangaza na mimi nimekubali nitakuwa Balozi wenu,”amesema.

Aidha, Sheikhe Rajabu amesisitiza umuhimu wa jamii kujikita kuhakikisha watoto  wanawapa elimu bora kwani Mwenyezimungu yupo pamoja na wale wenye kutafuta.

“Wekezeni katika elimu na bahati nzuri watu wa Kondoa mmepata watu wazuri Mbunge wenu na Mkuu wenu wa Wilaya ni watu wazuri jikiteni katika kutoa elimu kwa watoto wenu,”amesema.

Kwa upande wake mwanafunzi wa shule hiyo, Najma Lubuva amewapongeza walimu na wamiliki wa shule hiyo kwa  kuwawekea mazingira mazuri ya kujisomea ambapo amedai atahakikisha mafaulu mitihani ili ndoto yake ya kuwa Daktari iweze kutimia.

Mwanafunzi huyo amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza idadi ya shule katika vijiji ili wahitimu wa kidato cha nne waweze kuongezeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles