32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Jamii yatakiwa kutoa kipaumbele kwa mtoto wa kike

jamii
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Eda Sanga

Na Christina Gualuhanga, DAR ES SALAAM.

JAMII imetakiwa kumpa kipaumbele mtoto wa kike kwa sababu ana uwezo wa kuendelelza vizazi vijavyo.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake  Tanzania (TAMWA),  Eda Sanga, wakati akifungua mafunzo ya usalama barabarani, sambamba na maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa, ambapo amesema ipo haja ya mabadiliko ya mifumo ya kisheria ambayo imekuwa kikwazo kwa mtoto wa kike.

Alisema ajali za barabarani zinapotokea mtoto wa kike anaathirika kwa kiasi kikubwa baada ya kuondokewa na wazazi wake pindi ajali inapotokea na kumsababishia kubeba mzigo wa kutunza familia akiwa bado mdogo.

Eda alisema pia ipo haja ya kuharakisha mchakato wa kubadilisha sheria kandamizi zikiwemo mila potofu ambazo zimekuwa zikididimiza maendelelo ya mtoto wa kike.

“Nina imani mtoto wa kike akipewa nafasi anaweza hivyo ni lazima jamii iendane na wakati,” alisema Eda.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi  zilizokubali kuingia mikataba ya kimataifa kulinda haki za watoto, hata hivyo Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 bado ni kandamizi.

Naye Mratibu wa Programu ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania, Jones John alisema maadhimisho ya siku ya mtoto kimataifa yanawakumbusha wanaharakati kupigania haki bora ikiwemo kuikumbusha serikali kubadili vikwazo vinavyochangia ukiukwaji haki za watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles