25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 23, 2021

Jamii yatakiwa kuepuka matumizi dawa za kulevya

CHRISTINA GAULUHANGA -DAR ES SALAAM

JAMII imeshauriwa kuepuka matumizi ya dawa za kulevya kwakuwa zina madhara mengi ikiwamo wanawake watumiaji kuharibu mfumo wa hedhi na kuharibika kwa mimba.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam katika Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa,  Ofisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Makosa ya Jinsi nchini Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Ched Ngagunga alisema katika maonyesho hayo wameyatumia kutoa elimu alimu ya athari za dawa za kulevya na mbinu rahisi za Kudhibiti matumizi ya dawa hizo kuanzia ngazi ya familia.

Alisema katika maonyesho hayo zipo dawa za aina mbili za viwandani na mashambani ambapo nyingine inasisimua misuli na nyingine inafanya mtumiaji kuzubaa au kusinzia.

Alisema madhara ya matumizi ya dawa hizo za Kokeini na Heroini ni makubwa na yanafanana ambapo wengi wanapenda kutumia Heroini kwa kuwa inapatikana kwa bei nafuu.

“Matumizi ya dawa hizi yana madhara makubwa kwa wanawake  kwani yanaharibu mfumo wa uzazi, mimba pia kwa wanaume wengi wanakosa hamu ya tendo la ndoa na hata wanaopenda tendo na hata anayeitumia kokeini anapenda ngono mara kwa mara japokuwa inakuwa haina nguvu,” alisema Ngatunga.

Alisema Kokeini nyingi zimekuwa zinatoka ukanda wa Amerika Kusini yaani Brazil, Mexico, Peru, Colombia na kwingineko.

Alisema watumiaji wa dawa hizo wengi huwa wachangamfu kupita kiasi halafu wanakuwa na ndoto ambazo hazipo pia wanaangaalia kwa kutanua sana mbinu ya hicho. 

Ngatunga alisema pia kwa mtumiaji wa mirungi ni rahisi kupata vidonda vya tumbo, sarani ya koo, meno kuoza, kuharibu figo, kukosa hamu ya kula, kushindwa kufanya tendo la ndoa na kukosa usingizi.

Ngatunga alitoa tahadhari kwa jamii pindi wanapokuja safari kutokubali kupewa chakula cha aina yeyote ikiwamo keki, madhara au vinywaji.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,796FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles