33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Jamii yaaswa matumizi ya simu janja

Na FARAJA MASINDE – DAR ES SALAAM

ILI kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwa watoto, wazazi wametakiwa kuhakikisha simu janja (Smartphone), wanazowanunulia watoto wao kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali mtandaoni wanaweka programu maalumu kudhibiti maudhui yasiyoyofaa kwa watoto wao.

Akizungumza na Dar es Salaam jana, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Broad Security Technologies inayojishughulisha na uuzaji wa programu za kudhibiti uhalifu mtandaoni, Johnson Chaulaya alisema wazazi wanapowaachia watoto simu kwalengo la kujifunza zipo tarifa hujitokeza katika simu hiyo, wakati mtoto akiitumia jambo ambalo humpotezea mwelekeo wa kile anachokifanya na kujikuta akijifunza qmambo yasiyo stahili.

“Mara nyingi tunaona wazazi wakiwanunulia simu watoto wao au mara nyingine kuwaachia zao ili kucheza gemu au kujifunza masomo au kuangalia katuni.

“Sasa yapo mambo mtoto anaweza akafungua pasipo mzazi kujua na kuanza kufuatili sasa ili kudhibiti hayo tunashauri kabla ya kumpa mtoto simu hakiisha umeweka program ya kudhibiti maudhui usiyoyataka mtoto kufuatilia katika mtandao hii itasaidia kuwa na watoto wenye mtizamo bora zaidi,” alisema.

Akizungumzia namna ya kudhibiti wizi mtandaoni,alisema pia zipo programu za kudhibiti kurasa zinazotumiwa na wezi kupenyeza katika mitandao kwa lengo la kuiba taarifa za siri kwa lengo la kufanya uhalifu.

“Lazima wafanye utafiti wa program bora zitakazowasaidia,pia ni vyema kuakikisha kama un akifaa chako cha mawasiliano simu au kompyuta na vingine vinavyofanana na hivyo unaziwekea program za kuilinda chombo chako dhidi ya taarifa zako,”alisema. Kwa mujibu wa Malaka ya MawasilianoTanzania (TCRA), mwaka 2017 Tanzania ilivunja rekodi ya ukuaji wa sekta ya mawasiliano, baada ya kufikisha watumiaji wa intaneti milioni 23 kwa mwaka, kiwango ambacho ni zaidi ya mara tatu ya kile kilichorekodiwa miaka

mitano iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles