Na KHAMIS SHARIF-ZANZIBAR.
MAHAKAMA Kuu Zanzibar, imeitaka jamii, kuacha kuwashutumu majaji na mahakimukuwa wanajihusisha na vitendo vya kula rushwa katika kesi za udhalilishaji, badala yake waelewa kuna ugumu mkubwa wa uendeshaji wa kesi hizo.
Kauli hiyo, ilitolewa visiwani Zanzibar na Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar, Mohamed Ali Mohamed, alipojibu hoja za baadhi ya wajumbe, waliohudhuria uwasilishwaji wa rasimu ya utoaji wa huduma kwa umma.
Alisema alisema si sahihi kuona jamii inalalamikia au kuwashutumu watendaji wakuu wa ngazi ya mahakama wanakula rushwa kwenye kesi hizo.
Alisema lazima jamii iamini kuna ugumu wa kesi hizo katika uendeshaji hadi hatua za kutoa uamuzii sahihi kisheria.
Akitoa mfano wa kesi zainazowaumiza vichwa majaji na mahakimu, alisema wazazi kubaka au kulawiti mwanawe, kaka na mdogo wake, au mjomba na shemeji kwa kuwadhalilisha watu wao wa karibu.
Alisema ugumu zaidi,huanzia wakati wanapotakiwa kutoa ushahidi, mtoto huona au watoto huona wazi wana wanafunga wazazi wao miaka 30, huanza kupotosha ushahidi.
Alisema siku zote kesi za aina hiyo,jamii husubiri kwa hamu hukumu yake.
Alisema wapo baadhi ya majaji na mahakimu, wamekuwa wazito kwenye utoaji wa hukumu katika kesi hizo.
Akiwasilisha rasimu ya mkataba wa utoaji wa huduma kwa umma, mtoa mada Maulid Shaib Abdalla, alisema madhumini makuu ya mkataba huo, ni kutoa huduma zilizobora na kwa wakati kwa wananchi wote.