Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
“Ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha kwamba anaimarisha amani duniani ambayo itakuwa ni alama kwa kizazi kijacho na kuifanya dunia kuendelea kuwa sehemu salama ya kuishi,” amesema Man Hee Lee ambaye ni Mwenyekiti wa HWPL kupitia hotuba yake ya maadhimisho ya miaka saba ya azimio la amani.
Akizungumza kwa njia ya video Mwenyekiti wa HWPL, Man Hee Lee katika maadhimisho ya saba ya tangazo la Amani na kuzuia silaha uliofanyika juzi jijini Dar es Salaam kiongozi huyo alisema kuwa HWPL imesaidia kuleta amani.
“Tukiwa na mpango kazi kila mmoja wetu anaweza kufanikisha kuwapo kwa amani kwenye nchi zetu,” amesema Lee kupitia hotuba hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Mohammed akizungumza katika mkutano huo kuhusu hali ya amani nchini amesema kuwa amani ni ishara ya uhuru na UVCCM mkoa wa Dar es Salaam kwa kulitambua hilo ndiyo sababu wamekuwa wakishiriki kwenye warsha kama hizo na kwamba kwani kupitia hili tutaweza kuifikia jamii kupitia nyanja mbalimbali katika kuhakikisha kuwa kila mmoja anatambua umuhimu wa maani.
“Uvccm Dar es Salaam itaandaa mjadala wa wazi utakaoshirikisha viongozi wa dini ambapo watazungumzia kuhusu umuhimu wa amani. Pia tutashawishi Serikali kuangalia namna gani somo la amani linaingizwa kwenye mtaala ili kusaidia wanafunzi kufundishwa kuhusu amani wakiwa shuleni hususan somo la Uraia.
“Sote ni mashahidi kwamba Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia mazungumzoa yake na viongozi wa vyama vya siasa ikiwamo kuruhusu mikutano ya hadhara ni wazi kuwa ni kichocheo cha amani pia amekutana na viongozi wa dini nchini ambapo ameweza kuzungumzia juu ya umuhimu wa amani,” amesema Nasra.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Clara Peter alisema kuwa ni muhimu kutengeza jamii ambayo itaruhusu vijana kufanya maamuzi kuhusu kupanga uzazi na afya ya uzazi kwa ujumla na kwamba hayo hayawezi kufanikiwa iwapo hakutakuwa na amani.
“Kama Mungu angefanya hivyo basi wote tusingekuwa hapa, mfano kuliibuka wimbi la mauaji miaka ya 2000 kipindi kile nikiwa mdogo Kaskazini mwa Tanzania ulikuwa kila ukiamka asubuhi unasikia flani amekufa, hivyo hapo unakuwa unajua kuwa kesho ni mimi, hapakuwa na amani.
“Hivyo, kuwawezesha vijana inasaidia kuondokana na vitendo vya kihalifu na hivyo kuchochea ukosefu wa amani,” amesema Clara.
Upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum alisema kuwa hakuna vita kubwa kama ya amani, hivyo watu wote wanapaswa kushikamana Tanzania.
“Tujitahidi kuwa na amani na leo hatuna hofu tena ya vita ya ukabila na si jambo rahisi bali ni kazi kubwa imefanyika leo Sheikh hamuogopi mchungaji, mwanzo haikuwa hivyo tulianza kwa kazi sana viongozi wa pande zote walipata shida hiyo wewe unakaa na yule n.k leo ni miaka 13 tunaenda vema sasa.
“Naamini kwamba mkutano wetu huu ni ibaada na Mungu atatulipa kwa hili, tuwe tayari kuhakikisha kwamba tunapigania amani siyo ya tanzania tu bali dukia nzima, silaha za maangamizi hapana. Lazima tuungane. Dunia inataka amani amabyo lazima tujipange.Â
“Vijana ni bomu kubwa sana iwapo litaachwa bila kazi ya kufanya kwani ndio wanaweza kutumika vibaya endapo hako zao hazitazingatiwa. Tutaendelea kushirikiana kwa pamoja ili kuona kwamba amani ya Tanzania amani ya dunia nzima ni jukumu la kila mtanzani,” amesema Sheikh Salum.