25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Jamii itambue mchango wa mwanamke kwenye uchumi

LICHA ya juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na serikali na wadau wa maendeleo nchini  kuhakikisha inakuwapo sera nzuri na mifumo ya kuwezesha ukuaji uchumi kupitia sekta ya fedha lakini bado mchango wa mwanamke hauonekani.

Hata hivyo, serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), nayo imeendelea kutoa miongozo ya kuhakikisha Malengo ya Milenia yanafikiwa ifikapo mwaka 2015 ili Watanzania takriban asilimia 50 waweze kufikiwa na huduma za  benki.

Ripoti ya Maendeleo ya Watu Afrika  ya  2016  kuhusu  usawa  wa  jinsia inafuatia pamoja na ile ya Maendeleo ya Watu  Afrika  ya  mwaka 2012  iliyoangazia  umuhimu wa kuhakikisha usalama kwa  waafrika  wote. 

Ripoti zote mbili zina lengo moja la kushughulikia kile kinachoonekana kuwa   ni   utekelezaji   wa   ajenda   zilizokuwa    bado    kukamilishwa    katika  mwelekeo  wa  maendeleo  ya       Afrika. 

Yote  mawili  yametambuliwa  kama  vipaumbele  muhimu  kwa  serikali  barani Afrika.

Ili  kushughulikia  upungufu huo, ripoti hiyo inachukua njia ya uchumi jamii katika masuala ya  usawa  wa  jinsia  na  uwezeshaji  wanawake barani Afrika ikiwamo Tanzania.

Kutokana na hali hiyo, sasa ni wakati kwa Tanzania kuweka mkazo wa  sera  na  programu  katika  kutumia  vipaji vya wanawake kuleta msukumo wa   uchumi na   jamii kwa     maendeleo  jumuishi na  endelevu  zaidi. 

Kwa  maelezo  rahisi,  kuongeza  kasi ya usawa wa jinsia ni jukumu muhimu   la   serikali,   likihusisha   jitihada     za     sekta     mbalimbali     zikiwamo   taasisi   za    taifa,        watendaji    wasio    wa    kiserikali,     vyama     vya      raia     na   sekta   binafsi. 

Vivyo   hivyo,   kushughulikia   usawa   wa   jinsia   kwa   namna   pana      kama   hiyo   kunaunganisha     na     kuimarisha     ajenda  motomoto  ya  Malengo  ya  Maendeleo     Endelevu     (SDGs),     ambayo   serikali   za   Afrika   na   jamii   ya    mataifa   kwa   pamoja   wamejiwekea kwa miaka 15 ijayo.

Njia  pana  katika  kuleta  usawa  wa  jinsia pia itaimarisha mafanikio ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika.  Ripoti  hii  ya  Maendeleo  ya  Watu  Afrika  ya  2016,  kwa  hiyo,  inatoa  muundo-kazi   wa   utekelezaji   wa   SGD.

Hatua hiyo sasa inamfanya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kuona umuhimu wa sera   za uchumi wa nchi kutambua mchango wa mwanamke kwenye uzalishaji mali na ukuaji wa uchumi wa taifa.

Tunaunga mkono uamuzi  huo wa Makamu wa Rais Samia, kwa sababu  ni ukweli ulio wazi kwamba wanawake wengi wamekuwa wakishiriki kujenga uchumi kupitia sekta isiyo rasmi lakini bado wamekuwa hawatambuliki kwenye sera.

Hatua ya kuwapo   mikakati mbalimbali ikiwamo pia ile ya Benki ya TPB kuja na Akaunti ya Tabasamu ambayo ni mahsusi kwa wanawake ni sehemu ya mkakati wa kumuwezesha mwanamke kama kiungo muhimu kwenye uchumi wa nchi yetu.

  Tunajua kwamba wanawake ndiyo wazalishaji wakubwa na wengi wao wanamiliki viwanda vidogo na vya kati lakini bado mchango wao hautambuliki kwenye ukuaji wa uchumi.

Hatua hiyo inaweza kuwa kile alichokiona Makamu wa Rais Samia kwamba hata sera zetu bado hazijatambua hilo na sasa umefika wakati kwa mamlaka za serikali kuliona hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles