30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Jamii inahitaji kuhudumiwa na Tume ya Haki za Binadamu

Na ASHA BANI, DAR ES SALAAM


MTANDAO wa watetezi wa Haki za Binadamu jana ulitoa waraka ukimkumbusha Rais Dk. John Magufuli, mambo muhimu juu ya hali ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini.

Miongoni mwa mambo hayo muhimu ni pamoja na kuwepo kwa uteuzi wa viongozi kwenye muundo kama ambavyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya mwaka 2001 inavyoelekeza.

Muundo huo ni; kuwepo kwa Mwenyekiti wa Tume, Makamu Mwenyekiti, ambaye atateuliwa kwa kuzingatia kanuni kwamba endapo mwenyekiti ni mtu anayetoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, yeye atakuwa ni mtu wa kutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano.

Pia kuwepo kwa Makamishna wengine wasiozidi watano ikiwa ni pamoja na Makamishna Wasaidizi, Katibu Mtendaji wa Tume ambapo pia ni muhimu kutambua kwamba tume inaongozwa na Mwenyekiti ambaye anateuliwa na Rais.

Lakini pia Tume ina Makamishna na Makamishna Wasaidizi ambao nao wanateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Kamati ya Uchaguzi na hao ndio watakuwa viongozi wa juu wa Tume ambao kuwepo kwao kunasababisha Tume kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Kutokana na kumaliza muda wao tangu Januari mwaka huu, hakuna kiongozi mwingine aliyeteuliwa hali ambayo inaweza kudhorotesha hali ya utetezi wa haki za binadamu nchini.

Kutokuwepo kwa viongozi hao kunaweza kuwepo madhara mbalimbali ikiwemo masuala mengi ya haki za binadamu kutochukuliwa hatua kutokana na kutokuwepo kwa tume hiyo kisheria.

Athari nyingine ni THRDC na wadau wengine wa haki za binadamu sasa hawana nafasi ya kushirikiana na tume katika maeneo mengi ya haki za binadamu.

Mbali na hayo, mtandao huo pia umezungumzia hali halisi ya kifedha jambo ambalo kama Serikali inatakiwa kuliangalia na kulitilia mkazo kuweza kukamilisha na kutekeleza bajeti yake kama ambavyo imepanga.

Kwani kwa kufanya hivyo kutawarahisishia Tume kuweza kufanya kazi zake vizuri.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju, aliwaeleza wanaharakati hao kuwa wanatafuta umaarufu, hivyo ni vyema suala hilo likaangaliwa kama litakuwa na manufaa.

Anasema kufanyika kwa uteuzi huo endapo mchakato utakamilika wa kuwapata viongozi hao, basi kufanyike haraka kama ambavyo Serikali imeahidi ili kuipa uhai tume iweze kuwa na meno ya kulisaidia taifa katika masuala ya harakati na utetezi wa haki za binadamu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles