26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Jamii iendelee kuelimishwa kukomesha mauaji, ubakaji

MWANDISHI WETU, LINDI

KUMEKUWA na taarifa ya kuendelea kwa vitendo vya uhalifu hasa mauaji na ubakaji katika maeneo mengi ya nchi, japokuwa Serikali imekuwa ikijitahidi kukomesha tabia hiyo.

Juhudi za Serikali zimekuwa zikihusisha vyombo vya usalama na vyombo vya sheria kwa kuhakikisha wote wanaobainika kujihusisha na mauaji wanashugulikiwa na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Taasisi za kidini pia zimekuwa zikiendelea kukemea kwa nguvu zote kwa waumini wao kuhusu vitendo hivyo vya kukatili uhai wa watu wengine ambavyo vimekatazwa katika vitabu vyote vitakatifu.

Pamoja na juhudi zote ambazo zimekuwa zikiendelea, huku adhabu kali zikitolewa kwa wale wanaobainika kujihusisha na vitendo hivyo, bado vitendo hivyo vimeendelea kuripotiwa katika maeneo mengi ya nchi hivyo kuonesha uwepo wa haja ya kupanua wigo katika kutoa elimu na kuishirikisha jamii zaidi.

Ni hivi karibuni mkoani Lindi, jeshi la Polisi mkoani Lindi limeripoti kuwa limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa mauaji, Salum Ibrahimu ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mnolela Halmashauri ya Mtama mkoani humo anayetuhumiwa na kesi ya mauaji tangu mwaka 2018.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Stanley Kulyamo anasema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 17, 2018  mchana katika Kijiji cha Mnolela mashambani  ambapo mtuhumiwa huyo alimshambulia  Issa Selemani ambaye kwa saa ni marehemu.

Anaeleza kuwa mtuhumiwa huyo alimshambulia marehemu  kwa kumkata mapanga kichwani na kumsababishia majeruhi makubwa na baadae kufariki dunia akiwa njiani alipokuwa akipelekwa hosipitalini.

Kamanda Kulyamo anaeleza kuwa marehemu alikutwa na umauti huo wakati anaelekea shambani  kwa ajili ya shuguli za uzalishaji mali ambapo alipokuwa njiani katikati ya misitu ya shambani alisikia sauti ya kike ikiomba msaada.

Anasema marehemu alipoangalia sauti ilipokuwa ikitoka alimuona msichana ajulikanae kwa jina la Neema Said (13) (sio jina halisi) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mnolela akiwa anabakwa ndipo alipofanya maamuzi ya kwenda kutoa msaada.

Kamanda huyo anaeleza kuwa mbakaji alipoona marehemu anaelekea upande wake alimjeruhi msichana kwa kumkata kwa panga shingoni na baadae kumfata marehemu na kuaza kumshambulia kwa kumkata kata mapanga kichwani  na panga hilo hatimaye kumsababishia kifo akiwa njiani akipelekwa hospitali.

Aidha Kamanda Kulyamo anawaeleza waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kutenda kosa hilo alifanikiwa kutoroka ndipo Juni 30, 2020 alikamatwa akiwa katika Kijiji cha Mbuta akiwa amejificha mashambani.

Anasema jeshi hilo pia linamshikilia linamshikilia  Issa Hassan Maskati (24)  Mkazi wa Muungano Mnazi moja Manispaa ya Lindi mkoani hapo kwa tuhuma za wizi wa  pikipiki.

Anaeleza kuwa katika tukio hilo lilitokea Juni 16, 2020 majira ya saa 6:30 mchana maeneo ya Mnazi Mmoja  Manispaa ya Lindi mkoani humo mtuhumiwa akiwa na pikipiki iliyoibiwa katika Kijiji cha Nanganga wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Kamanda Kulyamo anasema baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi kijana huyo alionekana ni mwizi mzoefu na aliweza kutaja pikipiki zingine alizowahi kuiba na kuziuza sehemu mbali mbali.

Anasema Piki piki ya kwanza ilipatikana huko kilanje lanje kwa Sharafi Ally, (20) Mkazi wa Kilanjelanje na alipohojiwa alikiri kuwa kweli pikipiki hiyo aliuziwa na Issa Hassan pikipiki hiyo haina namba bali ina cheses No.LBR5PJB54H9000217 na Engine No.SL..157FMI 16974532 Nyekundu na pikipiki nyingine yenye MC.88 AUL SANLG Nyekundu yenye Chassis No.LBRSPJB51J9004439 Engine namba haisomeki hii ilipatikana kwa  Halid Mawewe (27) Boda boda Mkazi wa Mandawa kilwa.

Kutokana na kuendelea kuwepo kwa uhalifu huu hasa ubakaji unaoambatana na mauaji, pamoja na wizi wa mali na kuduru mwili hatua zaidi zinahitaji kuchukuliwa kwa kuwashirikisha wanajamii wote.

Wanajamii hawa wanatakiwa kupewa elimu kuhusu kuepuka kushiriki katika vitendo hivyo na kutoa taarifa kw awakati ili kuzuia wahalifu wa aina hii kuendelea kutenda uhalifu na kuathiri utu, mali na maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles