26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Jamhuri yaomba mahakama itoe hati ya kumkamata Tundu Lissu

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Upande wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi  inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wahariri wa gazeti wa la Mawio, wameomba Mahakama itoe hati ya kumkamata Lissu.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amewasilisha maombi hayo leo Jumatatu Februari 25, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Wankyo amedai mshtakiwa anaonekana akizunguka nchi mbalimbali akitoa mihadhara na huko Ubelgiji anakodaiwa yuko Hospitali haijaelezwa yuko hospitali gani.

“Kama itafaa Mahakama iamuru mshtakiwa Lissu akamatwe maana hayupo hospitali kama inavyodaiwa hapa mahakamani,” amedai.

Hata hivyo, Hakimu Simba alikataa maombi hayo na kuwaonya wadhamini kukumbuka majukumu yao ya kuhudhuria mahakamani na kutoa taarifa za washtakiwa.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Lissu na wenzake Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob, wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,424FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles