25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Jamhuri yakata rufaa kupinga Tido Mhando kuachiwa huru

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Siku tatu tangu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando aachiwe huru upande wa jamhuri  umekata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mahakama hiyo ilimwachia huru Mhando na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye alisema sababu za kumwachia huru kuwa ni mikataba minne aliyoingia haikuwa na nguvu ya kisheria kwani haikusainiwa na wahusika akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Lakini Jamhuri wanadai mashtaka yao ni hayo hayo kwamba mikataba hiyo iliingiwa bila kufuata utaratibu.

Pia wanadai kwamba kuingiwa kwa mikataba hiyo isiyofuata utaratibu kulisababisha Kampuni ya Channel Two Group kufungua kesi na Serikali ikalipa mawakili Sh milioni 887.1 ambayo ni hasara iliyosababishwa na mshtakiwa.

Katika kesi hiyo Tido alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles