25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Jamhuri yafunga ushahidi kesi ya Mdee

Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), wamefunga ushahidi wakiwa na mashahidi watatu.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kusikilizwa.

Wankyo alidai baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu wa upande wa mashtaka, wameona wafunge ushahidi.

Baada ya kudai hayo, Hakimu Simba aliwapa siku 14 upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao kama mshtakiwa huyo ana kesi ya kujibu au la na alitoa siku 14 kwa upande wa mashtaka kuwasilisha pia hoja za za majumuisho.

Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili Mosi kwa kutoa uamuzi kama Mdee ana kesi ya kujibu au la.

 Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mtaa wa Ufipa, Wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya Rais Dk. John Magufuli kuwa “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki”.

Kwamba maneno hayo yangeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.  

 Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles