31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Jamhuri yadai Mbasha alibaka ndani ya gari

Emmanuel Mbasha
Emmanuel Mbasha

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

UPANDE wa Jamhuri umedai mume wa mwimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha (32), alimbaka shemeji yake wakiwa ndani ya gari Mei 25, mwaka huu.

Hayo yalidaiwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, wakati Mbasha alipokuwa akisomewa maelezo ya awali dhidi ya mashtaka mawili ya ubakaji yanayomkabili.

Maelezo hayo yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi, Wilberforce Luhwago na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga.

Katuga alidai Mei 23, mwaka huu mke wa mshtakiwa, Flora Mbasha hakuwepo nyumbani, mshtakiwa alibaki nyumbani na shemeji yake ndipo akambaka.

Alipotakiwa kujibu kama kweli ama si kweli, Mbasha alikiri siku hiyo mkewe hakuwepo nyumbani.

“Ni kweli mheshimiwa siku hiyo mke wangu hakuwapo nyumbaani, nilibaki na shemeji yangu lakini sikumbaka kama inavyodaiwa,” alisema Mbasha.

Katuga aliendelea kudai kuwa Mei 25, mwaka huu mshtakiwa na shemeji yake walikwenda kumtafuta mkewe, wakiwa njiani wakati wanarudi, Mbasha alimbaka shemeji yake huyo kwa mara ya pili ndani ya gari.

Mshtakiwa alikana kufanya hivyo. Upande wa Jamhuri uliieleza mahakama kuwa unatarajia kuita mashahidi wanne kwa ajili ya kutoa ushahidi.

Hakimu Luhwago alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 22 mwaka huu, kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji, anadaiwa kutenda makosa mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.

Katika shtaka la kwanza, inadaiwa Mei 23, mwaka huu katika eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria na akijua ni kosa anadaiwa kumbaka shemeji yake (jina limehifadhiwa).

Katika shtaka la pili, ilidaiwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam kinyume cha sheria, mshtakiwa alirudia tena kumbaka shemeji yake. Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

- Advertisement -

Related Articles

3 COMMENTS

  1. Kwa huyo dada toka mda wote huo hajasema kama kabakwa na kama kweli alibakwa siku ya tarehe 23 mei 2014 kwa nini?ASITANGAZE HADI ARUDIWE MARA YA PILI?
    Hao walikubaliana ila sasa ishu imekuwa kubwa kwao ndo maana wanatengeneza mwelekeo wa kumbwaga mwanaume baada ya BIBIE kupata mume mwingine,na akiwa mjamzito ni moja ya sababu hiyo.THE TRUTH WILL PREVAIL.

  2. We Flora, ama kweli wewe ndo nabii wa uongo waliotabiriwa kizazi hiki. We kweli kama ni mtumishi wa Mungu aliye hai, ulishindwa kumaliza hili jambo la aibu na mume wako?. Huduma uliyojipa mwenyewe ndo imeishia hapo kama ile ya Barnaba katika matendo ya mitume baada ya kuwa na ukaidi wa kutii.Usipande tena jukwaani eti unaimba, acha kunajisi kazi ya Mungu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles