JAMES MWAKIBINGA AMUOMBA RADHI DK. EMMANUEL NCHIMBI

nchimbi

Na Mwandishi wetu,


 

James Mwakibinga ambaye ni kada wa CCM aliyemshutumu Dkt Emmanuel Nchimbi kwa madai ya kujimilikisha floor nzima kwenye jengo la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na pia alisema Dkt Nchimbi ameuza kinyemela viwanja 200 vya Umoja wa Vijana vilivyoko Temeke, aomba radhi na kukiri kuwa taarifa hizo sio za kweli.

Anakiri kuwa taarifa hizo ambazo alizitoa tarehe 16 Agosti 2016, alizipata kutoka katika vyanzo visivyo rasmi na kuziamini kuona ni jambo la kizalendo kupaza sauti ili hatua zichukuliwe.

“Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa umoja wa Vijana Makao Makuu haujawahi kumiliki viwanja eneo lolote la Temeke na hivyo madai kuwa Dkt Nchimbi aliuza viwanja 200 haya ukweli wowote,” anasema Mwakibinga

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here