23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

JAMES COMEY: TRUMP HANA SIFA YA URAIS

WASHINGTON, MAREKANI


ALIYEKUWA Mkuu wa Shirika la Upelelezi Marekani (FBI) James Comey, ameendelea kumshambulia Rais wan chi hiyo, Donald Trump akisema hana maadili ya uongozi kushikilia wadhifa huo na huwachukulia wanawake kama ‘kitoweo ‘.

Awali Jumamosi Comey wakati akitangaza kitabu chake kipya kijulikanacho kama ‘A Higher Loyalty’ aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa Trump ni mtu mwovu na asiye na misimamo.

Safari hii akihojiwa na Shirika la Habari la ABC, Comey aliyefukuzwa na Trump mwaka jana alisema rais huyo huzusha uongo kila wakati na huenda anazuia haki kutendeka.

Saa chache kabla ya mahojiano hayo kurushwa, Rais Trump alimshambulia Comey kwa kile alichosema kuzusha ‘uongo mwingi’.

Comey amekiambia kipindi cha ABC Jumapili usiku: ‘Siamini madai kuwa ana matatizo ya akili au yu katika hatua za kwanza kuugua ugonjwa wa kusahau.’

‘Sidhani kama ana mapungufu ya kiafya kumwezesha kuwa rais. Ila ninachoamini hana sifa wala maadili ya kuwa rais’.

“Rais wetu ni lazima aheshimu na afuate maadili ambayo ndio mzizi wa nchi hii. La muhimu zaidi ni kuwa mkweli. Rais huyu hana sifa wala uwezo wa kufanya hivyo,” alisema Comey.

Baada ya mahojiano hayo kurushwa, Chama cha Republican anachotoka Trump, kupitia kamati yake ya taifa kilitoa taarifa ikisema hatua ya Comey kujitokeza mbele ya umma kunadi kitabu chake imeonyesha ‘utiifu wake wa juu amejilenga mwenyewe”.

“Kitu kibaya zaidi kushinda historia ya ukosefu wa nidhamu wa Comey ni kukubali kwake kusema chochote ili aweze kuuza vitabu kwa manufaa yake,” taarifa hiyo ilisema.

Sakata baina ya wawili hawa inaanzia wakati wa uchaguzi wa urais mwaka 2016, wakati Comey akiwa Mkurugenzi wa FBI, akiendesha uchunguzi wa madai kuwa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Democrat Hillary Clinton alitumia barua pepe binafsi katika masuala nyeti wakati akiwa waziri wa mambo ya nje.

Tofauti ya wawili hawa ilibainika zaidi Julai 2016 pale Comey aliposema Clinton hakuwa na makini kushughulikia barua pepe hizo, lakini FBI haitamshtaki, kitu kilichomkasirisha Trump, aliyesema mpinzani wake huyo katika kinyang’anyitro cha urais ni mhalifu aliyepaswa kuozea jela.

Alivyoingia madarakani, Trump akadaiwa kumlazimisha Comey aape kumtii, madai ambayo Rais ameyakana na akamfukuza kazi wakati FBI ilipoanza kuchunguza uhusiano wake na Urusi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles