27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

JALADA LA MKE WA BILIONEA MSUYA LAKWAMA KWA DPP

NA KULWA MZEE – DAR ES SALAAM


UPANDE wa Jamhuri umedai kwamba  jalada  halisi la kesi ya mauaji inayomkabili mke wa  bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake bado liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), linafanyiwa kazi.

Hayo yalidaiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, wakati kesi hiyo  ilipokuwa inatajwa.

“Mheshimiwa Hakimu jalada halisi la kesi bado liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka analifanyia kazi, naomba mahakama iahirishe kesi hii  hadi tarehe nyingine kwa kutajwa,” alidai Mwita.

Hakimu Simba alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 23, mwaka huu kwa kutajwa na washtakiwa walirudishwa mahabusu kwa kuwa shtaka hilo halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni mke wa marehemu bilionea Msuya, Miriam  na mfanyabiashara Revocatus Muyela, ambao  wanadaiwa kwa makusudi walimuua dada  wa marehemu bilionea Msuya, Aneth Msuya.

Inadaiwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo la mauaji  Mei 25,2016 maeneo ya Kibada Kigamboni, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,327FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles