24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

JAJI MUTUNGI AVUNJA UKIMYA HUKUMU CUF

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi  ametaka Watanzania kuepuka taarifa za upande mmoja zinazotolewa kwenye mitandao na badala yake watumie vyombo vya habari makini kupata taarifa zinazohusiana na ofisi yake.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na MTANZANIA,  ambapo alisema anashangazwa kuona jamii inakumbatia zaidi habari za mitandaoni ambazo baadhi hazina ukweli kuhusu yeye, kwa sababu kuna masuala yameelzwa bila kuzingatia mkisingi ya weledi.

“Kuna watu wamekuja ofisini kwangu wakijiita viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF),  lakini kimsingi sitambui kama ni viongozi kwa sababu tayari nilishatoa taarifa za kutotambua uongozi wao, wanadai walileta taarifa ya Mahakama.

“Sikuwepo ofisini kwa sababu nilikua mgonjwa. Lakini nashangaa wamekwenda kwenye kitandao ya kijamii wamesema maneno mengi ya upotoshaji kuwa nimejifungia ofisini na kukataa kupokea taarifa yao,” alisema Jaji Mutungi

Alipoulizwa sababu za kutilia shaka ujio wa maofisa hao wa CUF Jaji Mutungi alisema utaratibu wa kufikisha taarifa za mahakama unajulikana.

“Hata kama ningekuwepo ofisini tayari nilishatoa salamu kwa maofisa wangu kuwa hao watu waandike barua kueleza malalamiko yao lakini si kuniletea taarifa ya mahakama.

“Siku hizi kila kitu kinaghushiwa hadi taarifa za Ikulu kuna watu wanaghushi, mimi nitaamini vipi kama kweli taarifa ile ilikua inatoka mahakamani? Mbaya zaidi wanaishia kueleza mambo kwa namna wanavyotaka wao kwenye mitandao ya kijamii, halafu ndugu zangu wanahabari mnazipokea kama zilivyo,” alisema.

Chama cha CUF kinakabiliwa na mgogoro wa ndani baina ya Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye anatambuliwa na msajili kama kiongozi halali pamoja na Katibu Mkuu wake Maalim Seif Sharif Hamad.

Baada ya kuripotiwa taarifa za uamuzi wa mahakama kuhusu kuzuia ruzuku kutopewa Lipumba, CUF upande wa Maalim Seif waliandika baru kwenda kwenye taasisi mbalimbali kuwafahamisha kuhusu hatua hiyo ya mahakama wakisisitiza kutotolewa kwa fedha hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles