JAJI MSUYA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

0
673

ASHA BANI na AUGUSTINO LACHUO (TURDACO)

ALIYEKUWA Jaji wa Mahakama Kuu ambaye amejiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na ugonjwa wa kiharusi uliokuwa ukimsumbua kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Kelvin Msuya mama yake alianza kuugua  Julai mwaka jana kwa ugonjwa wa kiharusi ambapo alipelekwa India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Alisema mama yake alikaa India kwa mwezi mmoja na baadaye alirudi nchini na kuendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na katika Hospitali ya Herbet Kairuki iliyopo Mikocheni Dar es Salaam.

“Mama alianza kuugua mwaka jana na hali yake ilivyokuwa mbaya alikimbizwa nchini India kwa matibabu lakini baadaye alirudishwa nchini na kuanza matibabu katika hospitali ya Kairuki (Herbet) na Muhimbili ikiwa ni pamoja na matibabu ya mazoezi ya mara kwa mara ,’’alisema Kelvin.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here