25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Mkuu atoa neno kwa majaji wapya

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma, amewataka majaji wapya walioapishwa leo, kuzingatia sheria na kufanya katika kutoa uamuzi bila kujali hali ya mtu.

Aidha, amewataka kufanya biashara halali ili kuepuka mgongano wa kimaslahi utakaosababisha watu wengine wasipate haki.

Jaji Mkuu amesema hayo leo Jumanne Januari 29, katika hafla ya kuapishwa kwa majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani walioteuliwa na Rais John Magufuli, Januari 27, mwaka huu.

“Kama Jaji ana bodaboda na ikakamwatwa ukampigia Afande Sirro (Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro) ili isiende mahakamani hiyo haikubaliki,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Jaji Profesa Juma amempongeza Rais Magufuli kwa idadi kubwa ya majaji na kuongeza kuwa itasaidia kupunguza mzigo wa kesi anazosikiliza jaji mmoja.

“Uliniuliza unataka majaji wangapi, nikakwambia una majina 60 mezani kwako. Nashukuru ulipopata takwimu zetu wewe ulikuwa wa kwanza kunikumbusha hali ya majaji Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani si mzuri.

“Nawpongeza majaji wapya, nimesikiliza viapo vyenu kuonyesha utayari kwenda kutumikia jamhuri, tusianze baada ya hapa kuulizana nani anataka kubaki Dar es Salaam, utakuwa umekiuka masharti ya kiapo chako,” amesema.

Jaji Mkuu pia amewataka majaji hao kutambua kuwa Jaji ni mtu asiyelala, hana mwisho wa wiki wala sherehe bali siku zote yuko kazini na akiwa kazini hana msaidizi ni yeye na jalada yake tu.

“Ninyi ni majaji wa karne ya 21 kanrne yenye changamoto nyingi sana, ni vizuri huu muda mchache mtakaokwenda kukabidhi ofisi muanze kujiandaa kwa maisha mapya.

“Elimu endelevu ni muhimu, zamani tulikuwa tunaambiwa jaji anajua kila kitu, lakini hapa baada ya kiapo mtakwenda kozi kwa mwezi mmoja, kwa sababu mwananchi akikuona mara ya kwanza mahakamani hajui wewe ni Jaji mpya anajua wewe ni Jaji,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles