25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Jaji Mkuu asisitiza maadili mema kwa jamii

Na CHRISTINA GAULUHANGA

-DAR ES SALAAM

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, ameiasa jamii kujenga tabia ya kuwa na maadili mema kwakuwa ndio chanzo cha kutii sheria za nchi.

Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki Dar es Salaam katika futari iliyoandaliwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zuberi.

“Sheria zimetungwa, zinatakiwa kuzingatia maadili ya dini, hivyo ni vyema jamii ikasimamia maadili,” alisema.

Alisema maadili yakizingatiwa sheria itaweza kufanya kazi vizuri kwani hata maovu nchini yatapungua.

“Jamii ikizingatia maadili na sheria itaweza kufanya kazi yake vizuri, lakini kwa sasa maadili yamezidi kutoweka na kusababisha uvunjifu wa sheria na kupelekea kukosa misingi ya maadili kila kukicha,” alisema.

 Profesa Juma alisema viongozi wa dini mbalimbali wamekuwa wakifanya kazi kubwa katika kusikiliza na kutatua changamoto zilizopo ikiwamo kukemea vitendo vya uvunjifu wa maadili.

Alisema  suala la mirathi limekuwa likichukua muda mrefu mahakamani, lakini viongozi wa dini wamekuwa wakipatanisha katika misingi ya dini na kusaidia kupunguza migogoro inayojitokeza ndani ya jamii.

Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, alisema viongozi wa dini wana nafasi ya kuijenga jamii kimaadili na kuleta amani nchini.

Alisema viongozi wa dini wamekuwa wakihamasisha amani katika maeneo mbalimbali hali ambayo imeweza kupunguza migogoro kwa kiasi kikubwa.

Naye Mkurungezi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Diwani Athumani, alisema nchi itajengwa kwa misingi ya amani na upendo endapo watu wote wataungana na kukemea rushwa.

“Rushwa ni adui, hivyo ni jukumu letu kushirikiana kwa kuungana pamoja kukemea vitendo hivyo ili kufikia maendeleo,” alisema Athumani.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mufti Zuberi alisema anashukuru wameweza kukutana kwa pamoja wakati mwezi Mtukufu wa Ramadhani  ukielekea kumalizika.

“Ni furaha ya kipekee kwangu mimi binafsi na kwa jamii nzima tumeweza kujumuika pamoja,  tunamuomba Mwenyezi Mungu atujalie heri na baraka zaidi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles